Friday, September 11, 2009

Unakaribishwa Ushiriki Kujenga Kanisa

Mshiriki wa Kanisa hili ametuma ujumbe huu wa kutukaribisha tushiriki katika ujenzi huo:

Natumaini hamjambo. Kwa zaidi ya miaka 50 tangu injili ilipoingia mjini Bukoba tumekuwa na kanisa moja tu. Ni mpango wa kanisa kuongeza wigo wa kazi kwa kuongeza makanisa ndani ya mji wa Bukoba. Kwa kuanza tayari kanisa limetengwa lijulikanalo kama MAFUMBO SDA. Tuko katika harakati za ujenzi na bahati mbaya zaidi ya 50% ya washiriki wa kanisa hili jipya ni tegemezi.

Napenda kuwashirikisha ninyi rafiki zangu katika ujenzi wa kanisa hili kadri mnavyobarikiwa. Najua mna majukumu mengi, ila Mungu atawawezesha. Nimeambatanisha barua ya kanisa ya kuomba mchango pamoja na picha za jengo tunaloabudia kwa sasa. KWELI MUNGU WETU ANAAIBISHWA KWA NYUMBA HII DUNI YA IBADA!!!!

Akaunti ya kanisa ni [...]

[Mwandikie geustace78@yahoo.co.uk akutumie akaunti hiyo]

Asanteni sana na Mungu azidi kuwabariki.

Grace Eustace


KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO MAFUMBO
S.LP.319 BUKOBA SIMU: 2220677


Ndugu Mheshimiwa, Bi, Bwana,……………………………………………………..
Amani, Baraka na Neema zitokazo kwa Bwana aliye Mungu wetu viwe pamoja nawe. Amina.

YAH: OMBI LA MCHANGO KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA

Mpendwa tunaomba mchango wako wa hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa jengo la kanisa ambalo limeonyeshwa kwenye picha hiyo hapo juu. Hadi sasa tumekamilisha ujenzi hadi kufikia sehemu kubwa ya boma ambao umegharimu shilingi zipatazo 12,000,000/. Hivi sasa tunategemea kuingia katika hatua ya kuezeka paa. Tumekuchagua kwa matumaini ya kupata chochote kati ya hivi vifuatavyo na Bwana atakubariki: Mabati, Mbao, Fedha tasilimu pamoja na maombi (dua) yako.

Waweza kuwasilisha mchango wako kwa Kanisa moja kwa moja au kupitia kwa aliyekupatia kadi hii au kwa kutupigia simu ilionyesha hapo juu, nasi tutakufuata. Utapewa risiti ya Kanisa kwa matoleo yako.

Natanguliza shukrani, BWANA akubariki.

MCHUNGAJI HERI KUYENGA

Kanisa la Waadventista Wasabato-Mafumbo

Mimi………………………………………………….Natoa/naahidi kutoa…………………………………Tarehe……………………………………….Sahihi……………………

No comments:

Post a Comment