Tuesday, May 10, 2011

Ajali ya Kwaya ya Ambassadors of Christ

Hizi ni picha zilizopigwa tarehe 18 Julai, 2010 kwenye harusi ya Shima & Anjelina, kanisani Mwenge SDA na baadaye Mlimani City. Pamoja na hizo picha ni rambirambi za baadhi ya wadau walioguswa kwa namna moja au nyingine.

Hapa Faraja Sefue anaelezea kwa ufupi jinsi ajali ilivyotokea:

Poleni sana wanajukwaa.

Shima amenipigia simu sasa hivi, yeye yupo eneo la ajali huko Kahama na huu ndio mrejesho:

Ajali imetokea Tinde - Shinyanga vijijini saa mbili usiku jana tarehe 09/05/2011, gari waliyokuwa nayo wanakwaya ni left handed na mbele kulikuwa na lori limeharibika japo walikuwa wameweka majani kama ilivyo kawaida ya wa-TZ. Dereva akataka ku-overtake, hamadi lori la Iveco likawa linakuja na hatimaye ajali ikatokea. Dereva alijaribu kukwepesha gari na alishindwa wote walioumia walikuwa upande wa kulia. Marehemu ni Amos, Philbert na Gitale. Helicopter inakwenda asubuhi hii kuchukua majeruhi na kuwapeleka hospitali ya rufaa Kigali na ambulance inakuja kuchukua miili miwili ya Wanyarwanda pamoja na mwili mmoja wa Mtanzania kwenda Kigoma kwa mazishi.

Tuwaombee majeruhi wapate nafuu na kuendelea na kazi ya uinjilisti kwa njia ya nyimbo.

Mgune Masatu Wrote:

You know what?

I received a call from brother Opere in the middle of last night, all the way from Nairobi. Because I was sleepy, I couldn't understand and thought I was dreaming. But when I woke up in the morning, alas, it was no dream. I am sad. So sad.

Of all the folks, I will live to remember "Jimmy". Why? In 2008 at the retreat in Baraton, for those who were there can remember this. On the tour day (Thursday), all retreaters were given their lunches (take away) which included a bottle of soda. During the dinner, there was a condition that for one to be served some food, he/she had to return the bottle first. Unfortunately, the late Jimmy had lost his bottle, and so he was saying "Ooh kichupa changee" which is a Kinyarwanda for "Ooh my bottle" or in Kiswahili it's "aah chupa yangu!"

Again last year in July, the "Ambassadors of Christ Choir" were invited for a wedding ceremony right here in Dar es Salaam. The wedding took place at Mwenge SDA Church and followed by a reception at the famous Mlimani City Hall. When we were in the hall, I and my wife, when we were close to him, we called him simultaneously, "Hey Jimmy, Kichupa Changeeee," trying to remind ourselves of the Baraton's incident.

I am overwhelmed with all these fresh memories circulating on my mind. I am sad! Nimesikitika sana wapenzi. When I remember their famous song "Fuata Nyayo" and seeing Jimmy leading the "Fuataaaaa......." in his white shirt, oooh come on, I am speechless!

I am shaking while writing this. I may say that I need more prayers, but let's look at our lives and pray for the deceased' families, the church and everyone affected in one way or another.

Kaka Shima, pole sana. Najua msiba huu unakugusa moja kwa moja kwani utawakumbuka daima walivyotia nakshi kwenye harusi yako pale Mlimani City mwaka wa jana.

May God take the lead.

Sorrowfully yours,
Mgune Masatu.

Wema Wilson wrote:

O my God, ni habari ngumu sana kuamini! It's like Amos amekuja kufia nyumbani! Tena mkewe anafanya kazi Shinyanga. Huko kijijini Manyovu na Kigoma kwa ujumla hali ni tete kwa umuhimu wa Amos katika kijiji na kanisa kwa kujituma tangu akiwa ASSA, kwa sisi alikuwa kaka tena mentor mzuri so wenzenu nahisi tuna hali ngumu zaidi. Habari za sasa ni kwamba kuna helicopter inatarajiwa kuwasafirisha majeruhi kwenda Rwanda na Amos anasafirshwa kwenda Kigoma. Poleni sana wote mlioguswa, Mungu atufariji.
Wamepata ajali kilometa 70 to Kahama na 40 to Shinyanga. Chanzo kilichopo hospitali kinasema driver alikuwa ana-overtake akakutana na lori so wakabanwa na magari yote mawili. Waliokufa ni watatu. Mungu atusamehe tunaomuliza"Why this?" and "Why those?"

Kwa wale wasiowafahamu hao marehemu kwa sura,kwenye hii album mpya wamejipanga kwa kufuatana toka kushoto, mmoja(Philbert Manzi) anafanana sana na Kagame ,mwingine ni Gatare Ephraim(huwa wanamwita Jimmy) kwenye wimbo wa ebarua ndio ameshika bible,na wa tatu ni Amosi Phares mfupi kdg.

Majeruhi ni dada aliyeigiza kama mke aliyenyanyaswa kwa kutozaa, kijana aliyebebwa juu kwenye wimbo 'twapaona kwa mbali' na yule dada mweupe ana nywele fupi(anaonekana kama kaolewa). David Sando wrote:

Ni habari ya masikitiko sana, kwamba hawa waimbaji na marafiki wetu wa kweli!
Habari niliyokuwa nayo ni wanne, ila naambiwa, list ya walifariki niliyoelezwa kwanza ilikuwa ni Ephra, Patience, Amos and Pilbert, lakini muda si mrefu tena nikaambiwa Patience amenusurika ila yuko hoi kwa hiyo idadi imebaki 3 , ni kutoka kwa friends of jesus crew in Kigali and not confirmed 100%.


Hebu tuwaombee wanakwaya hawa katika kipindi hiki kigumu ?

Tafadhali kwa hili nimekuwa na wakati mgumu, mara tatizo kubwa kama ili linatokea na nakuwa na maswali mengi kama just out of curiosity question "Je, huu ni mpango wa Mungu au udereva mbaya wetu na miundo mbinu yetu mibovu"? Lengo sio kutafuta mbaya yuko wapi bali ni kujua kama ni tatizo ambalo liko zaidi upande wetu binadamu au ni vitu ambavyo ni non-modifiable?


Noah Mubiru wrote:

It is sad to inform you all of the death of some members of "Ambassadors of Christ Choir" - Remera church, Kigali. They were travelling from TZ where they had a show over the weekend. Those confirmed dead include Ephraim popularly known as Ephra, Philbert and Amos.

A few others are in critical condition. Please remember to mention them in your prayers! Leonard Chauka Wrote:

Hapa Duniani kila siku inabidi tuwe tayari kwa sababu wakati wote tunaweza kuondoka. Binafsi, habari hii ilinigusa sana. Kati ya wapenzi wa hii kwaya, nami ni mmoja wao. Nilifuatilia sana habari za ujio wao, PTA nilikuwepo na nikabarikiwa sana na nyimbo zao. Nilipopigiwa simu usiku wa manane na rafiki ambaye tulikuwa wote PTA kwa ajili ya kongamano lililoandaliwa na ACACIA Singers, niliumia sana moyoni. Matukio kama haya yatukumbushe kuendelea kuishi maisha yanayomtukuza Mungu wakati wote ili tuondoke Duniani na tumaini.

Mungu awapatie amani na uvumilivu mkubwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao, waimbaji wa Ambassadors of Christ waliobakia na wale wa Acacia Singers.

* Sikiliza nyimbo za Ambassadors kwenye blogu hii:

http://mtangazaji.blogspot.com/


Saturday, May 7, 2011

UZINDUZI WA ALBAMU MPYA YA NYIMBO!

SIKILIZA NYIMBO ZA KISABATO MTANDAONI

Tembelea blogu ya http://mtangazaji.blogspot.com/ usikilize moja kwa moja nyimbo za injili zinazoimbwa na vikundi na kwaya mbalimbali za Waadventista Wasabato!

BUILDING A CHURCH COMPLEX IN ARUSHA

This is a photo of Arusha Kati/Mjini SDA church that the photographer visited recently. According to him, it is the biggest project he has ever seen in our church in Tanzania. As you can see, the church members are currently working on final touches. May God continue to richly bless them. Amen.

Tuesday, May 3, 2011

Waumini Wazidi Kuongezeka Kanisani Ikizu

Wanafunzi 111 walibatizwa kwenye juma la maombi lililoendeshwa na Mchungaji Gerald Nyakrere, Mchungjai Shukurani Mutaki na Mchungaji Daudi Ndekeja katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ikizu. Kutokana na ongezeko la wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Ikizu Kanisa dogo lililojengwa zamani sasa halitoshi. Hivyo wanafunzi wanasalia nje wakati wa ibada kama inavyoonekana pichani wakati wa huduma ya Ubatizo. Picha hizi zilizotumwa mtandaoni na Baraka Joel Nyakrere ni changamoto tosha kwa Wanafunzi wa zamani wa Ikizu na marafiki wote wa Kanisa la Ikizu kusaidia ujenzi wa kanisa kubwa zaidi litakalotosheleza mahitaji ya waumini wapya.