Loading...

Wednesday, July 29, 2009

Mibaraka ya Makambi huko Morogoro Mjini!

Huu ni msimu wa Makambi. Sabato iliyopita nilipata mibaraka ya kujihudhurisha kwenye Kanisa la Katikakati ya Mji wa Morogoro. Hapo nilikuta Mchungaji wa zamani wa Mtaa wa Magomeni, Marko Marekana, akihubiri. Kabla ya Hubiri lake alimkaribisha Mkurugenzi wa Vijana kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato, Mchungaji Baraka Muganda, atoe Neno kwanza. Kama kawaida yake, kwa unyenyekevu, Mchungaji Muganda alikumbushia umuhimu wa kuiachia Mimbari kwa Mhubiri aliyejiandaa juma lote kisha akatoa Hubiri fupi kutoka kwenye Waraka wa Kwanza wa Petro 2: 4. Alitumia fungu hilo kujenga hoja ya Kithiolojia kuwa tunapaswa "Ku-Showoff", yaani, "Kujionyesha", ili kudhihirisha fadhili za Mungu. Pia alitujulisha kuwa anatarajia kuwa Musoma, Tarime kuendesha makambi yatakayojumuisha makanisa yote ya eneo hilo. Naye Mchungaji Marekana akamalizia na Hubiri Kuu lililojikita katika Yohana 4: 1 - 42 ambapo Mwanamke Msamaria ambaye hakukubalika katika Jamii yake alikutana na Yesu kisimani, akajionyesha kwa Wasamaria wenzake na kutangaza fadhili za Kristo kwa watu wote!

Vibanda vya Kisasa navyo Vilikuwepo Kuashiria kuwa Hakika haya ni Makambi!

Mchungaji Baraka Muganda Naye Alijihudhurisha na Kutoa Neno la Kufungulia Pazia!

Kwaya ya Magomeni Nayo ilitinga na Majoho Mapya na Kuitikia Wito wa Mchungaji!

Wakongwe wa Thisdaso Nao Hawakosekani kwenye Matukio Muhimu Kama Haya!

Wanafunzi nao Walikuwepo Tayari kwa Mojawapo ya Matukio Muhimu Sana Kambini!

2 comments:

  1. Inaonekana mlikuwa na wakati mzuri.

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa ujumbe na taarifa ya makambi ya Morogoro. Pia asante kwa taarifa mbalimbali kwenye blog yako. report ya Michael Ford kuuawa na Farm Tractor USA nimeisoma kutoka kwako, sikujua. Ninaishi maili 17 na nilimfahamu Michael na pia mama yake na familia yao. Nitapanga kwenda kuwapa pole familia. Asante. Elias

    ReplyDelete