Thursday, February 4, 2010

MHANDO AREJEA KUNDINI!

Wasabato mbalimbali niliowasiliana nao wamezipokea kwa furaha taarifa zilizochapishwa na Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, 3 Februari 2010, kuhusu Dakta Heri Mhando kurejea kanisani. Nami naungana nao katika furaha hii ambayo ilipotea wakati wa mjadala mkali wa Ukweli kuhusu Mchungaji Mhando kuanzisha Kanisa Lake la Wasabato Wapentekoste. Hakika kuna furaha mbinguni pia kama alivyonena Yesu kuhusu matukio mazuri kama haya!
AMEN

14 comments:

  1. What about those who can't read KiSwahili?
    Alvin

    ReplyDelete
  2. Namheshimu mno... Unyenyekevu huu utakuwa tu ni matokeo ya Roho wa Mungu ndani yake! :)

    ReplyDelete
  3. Wow! Hata mbinguni kuna furaha kubwa mdhambi mmoja anapoamua kutubu.
    Karibu sana Mwinjilisti Heri Mhando. Mungu bado anakupenda. Daima Mungu huwa ana njia zake za kushughulika na watu wake. Asante Baba kwa jina la Mwanao Yesu Kristo, kukutana na Mhando na kumrudisha. Hakika, Mungu hataacha kondoo wake hata mmoja apotee.
    Unaweza ukaona sasa upendo wa Mungu.
    Naomba roho chafu, manung'uniko, masengenyo, chuki, roho za uharibifu, za kuzimu, na na na ..... zisipate nafasi mtumishi wa Mungu aliye hai anaporejea. Amen!!!!!!

    ReplyDelete
  4. For an English version of the story visit http://phidza.blogspot.com/2010/02/welcome-back-dr-mhando.html

    ReplyDelete
  5. http://www.freemedia.co.tz/daima/ habari.php? id=12696

    Mwinjilisti Mhando arejea kwa Wasabato

    na Mwandishi Wetu

    Mwinjilisti wa Kimataifa aliyeanzisha mikutano mikubwa ya mahubiri ya kila mwaka katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, Dk. Herry Mhando,amerejea katika kanisa lake la awali la Waadventista Wasabato (SDA)nchini Tanzania alilojitoa mwaka mmoja uliopita.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk. Mhando alisema ameiacha rasmi huduma yake ya kujitegemea ya Uinjilisti na maombezi aliyoianzisha inayoitwa Seventh- day International Ministry (Huduma ya Kimataifa ya Wasabato)iliyovuta waumini wengi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo na kuamua kurudi kwa Waadventista Wasabato.

    “Huu sio uamuzi wangu binafsi. Ila ni uamuzi uliotoka kwa Mwenyezi Mungu, kwani tangu nilipoanzisha huduma hiyo nimefanya maombi ya kufunga kwa siku 415 mfululizo, nikila mlo mmoja tu wa jioni.

    “Roho wa Mungu akanielekeza kurejea nilikotoka, kule kwenye asili ya imani yangu ambako nililelewa vizuri ikiwemo kupata elimu yangu yote,”alisema Dk. Mhando.

    Alipoulizwa kama uongozi wa makao makuu ya Kanisa la Waadventista waSabato, una taarifa yoyote juu ya maamuzi yake hayo, alijibu kuwa tayari ameshaujulisha kupitia Askofu Mkuu wake, Mchungaji Joshua Kajula, na wanaendelea kushangilizwa na taarifa hiyo.

    Dk. Mhando alianza kufanya mikutano ya mahubiri ya wazi jijini Dar esSalaam iliyokuwa na mvuto mkubwa mwaka 1994 (viwanja vya Mnazi Mmoja)akitokea masomoni nchini Marekani na baadaye viwanja vya Jangwani katika miaka ya 1998, 2002, na 2006. Aliwahi pia kufanya mkutano maalumu wa kuombea Uchaguzi Mkuu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee mwaka 2005.

    Mwinjilisti Mhando amewahi kufanya mikutano mingine mikubwa katika bara la Afrika huko Kenya, Afrika Kusini, Zimbabwe, Uganda, DRC, Nigeria,Zambia, Namibia, Botswana, Malawi na Burundi. Nchi za Ulaya ni Uingereza, Uholanzi, Uswisi na Urusi. Mashariki ya mbali ni India na Ufilipino. Aidha, Marekani na Canada nako amewahi kuhubiri mara nyingi.

    Dk. Mhando aliwahi kuwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika Jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania(makao yake mjini Same) na Makao Makuu ya Kanisa hilo nchini (mjini Arusha) mwanzoni mwa miaka ya tisini kabla ya kwenda masomoni nchini Marekani.

    ReplyDelete
  6. Haleluyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!
    Mimi binafsi namshukuru Mungu kwa uamuzi ambao Dk.Mhando ameuchukua.Alikuwa ni mbaraka mkubwa kwa kanisa, naamini Roho wa bwana ataendelea kumtumia katika kulitegemeza kanisa la Kristo, hasa kipindi hiki tunapofunga historia ya Dunia.
    Mungu akubariki Dk Heri Mhando.

    ReplyDelete
  7. Kanisa letu la Magomeni lilipata mbaraka wa aina yake Sabato hii ya jana. Mhando alijumuika pamoja nasi kwenye ibada takatifu iliyoendeshwa na Mchungaji Kasika.Hakika amerejea kundini. Wapo waliorejea pamoja naye. Tunatumai wote watarejea pia. Amen.

    ReplyDelete
  8. Ni rahisi kumuita mwenzako mdhabi na kusema mafungu lakini je wewe umewafurahisha malaika mbinguni kwa kutubu dhambi zako?

    ReplyDelete
  9. Hizi ni habari njema. Nimsikiliza Dr. Mhando mara moja tu pale Bariadi Mjini na niliguswa mno na mahubiri yake. Inatia furaha kama nini kuona kuwa amerudi nyumbani.

    Karibu tena zizini mwa Bwana mtumishi wa Mungu. Nasi sote tuutumie wakati huu kujipeleleza na kurudi katika mbawa za mkombozi wetu. Hii ni siku njema!

    ReplyDelete
  10. Huwa najiuliza mfano wa shilingi ilyopotea lakini baada ya kupatikana, iliandaliwa sherehe ambapo naamini si shilingi ile ilitumika iliyopatikana bali hata na nyingine zilizokuwepo! Yote hayo ilikuwa ni furaha kufurahia kile kilichopotea na kisha kupatikana.
    Kwa mfano wa Bwana wetu Yesu Kristo, nashindwa kuuleza furaha iliyonafisini mwangu lakini zaidi mbinguni kwenyewe. Ubarikiwe Mtumishi wa Mungu Mhando kurejea kundini.
    Tahadhali kwetu sisi tulio-kundini, tujipelele.

    ReplyDelete
  11. TITUS TOSSY NI MFUASI WAKE PIA, NAMSIHI MUNGU KUMREJESHA MWINJILISTI TITUS TOSSY, TUKAZE MAOMBI.

    ReplyDelete
  12. kila tukio limpatalo binadamu ni ushuhuda kwa ajili ya wokovu wetu, naamini baada ya muinjilisiti H.Mhando kuwa nje ya kanisa kwa muda sasa anao ushuhuda mpana wa nini kiko nje na nini kiko kwa walio nje wakitoka ndani ya kanisa la Bwana wetu Yesu kiristo. Naliombea kanisa la Bwana ili tuwe na umoja kama baba alivvyo mmoja mbinguni.
    Naamini kazi ya Mungu itasonga mbele ili tuimalize kazi ya Bwana na Bwana arudi.
    ni vema kanisa likaamini ushuhuda wa kurudi kwake kundini na aendelee kuipeleka injili ya bwana duniani kote kupitia kanisa la waadventista wa sabato na injili ya ujumbe wa malaika wa tatu .
    nitafurahi sana kukiandaliwa mikutano mikubwa janngwani na ujumbe wa Bwana ukahubiliwa tena na tena ili watu wapate kuokolewa.Asante

    ReplyDelete
  13. namshukuru MUNGU kwa kumuonyesha njia ya kweli Dr. Mhando na kutambua kuwa kweli alikuwa amepotea na kutanga mbali na upeo wa mungu.Jukumu linakuja kwetu sisi wahumini tulio katika zizi la mungu yantupasa tuwe makini sana na tuzidi katika maombi,bwana akubaliki sana dr. mhando kwa uhamuzi ulioufanya.Ubalikiwe mtumishi wa mungu kutambua ukweli wa mungu.Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen!!!!

    ReplyDelete
  14. roho iliniuma sana kuufikiria mwisho wa mtumishi wa Mungu ambaye alifanya kazi kubwa sana ya kuwabadilisha watu kwa mibaraka mikuu aliyopewa na Mungu.hakika Mbegu ya Mungu haipotei ubarikiwe sana Dr. Mhando.Sasa tumebakisha kazi moja tu ya kuwaandaa watu wa Mungu kwa ajili ya marejeo ya Yesu mara ya pili na tuwakaribishe wengine kwa upendo.Mungu atubariki sana.

    ReplyDelete