Monday, June 28, 2010

SOMO LA UFUNUO KANISANI CHUO KIKUU - KUENDELEA JUMAMOSI 3 JULAI 2010 SAA 8 MCHANA (YOMBO LECTURE THEATRE)

MPANGO MPYA WA DINI YA DUNIA NZIMA (NEW WORLD ORDER)

UFUNUO 13: 3,4,6,8,9
Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu huyo joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, ni nani afananaye na mnyama huyu?Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie.


BAADHI YA SIFA ZA MFUMO WA DINI YA MPINGA KRISTO
Atafanya vita na watakatifu wazishikao amri kumi za Mungu na imani ya Yesu na atawashinda (Ufunuo. 13:7 )

Anaivuta dunia yote pamoja ili wampe heshima ya kiibada na kufuata mafundisho yake (Ufunuo 13:8)

Anafanya miujiza mingi na ishara kupitia mawakala wake ili kuihadaa dunia (Ufunuo 13:13)

Watakaokataa kujiunga na mfumo huu wa dini watanyanyaswa, kushitakiwa, kuteswa na hata kuuwawa (Ufunuo 13: 15)

Ana majina ya makubwa na ya makufuru (Ufunuo 13:5-6)

JINSI GANI MFUMO HUU UTAFANIKIWA KUANZISHA DINI YA DUNIA NZIMA?

MAFUNDISHO YA UONGO YATAPATA NGUVU INGAWA HAYATAONEKANA KOKOTE KATIKA BIBLIA

* SIKU YA IBADA ITABADILISHWA
* IMANI YA KUTOKUFA KWA ROHO
* MIUJIZA, UTAJIRI, BARAKA (NEW AGE THEOLOGY)
* UNENAJI WA LUGHA BANDIA (MEDITATION)
*MUZIKI WA DINI YA KIZAZI KIPYA/MAPAMBIO
*MUUNGANO WA MAKANISA NA DINI
*MATUMIZI YA NGUVU ZA DOLA KATIKA DINI

MUUNGANO WA MAKANISA UTAWEZEKANA/UMEWEZEKANA KUPITIA HARAKATI ZA UEKUMENE (ECUMENISM)

'Hatimaye kiini cha muungano wa kidini, kama Kanisa Katoliki linavyoelewa, ni umoja wa imani, ibada, na kutambua mamlaka ya kiroho ya Kasisi mkuu wa Roma' -Priest J. Cornell

'…umoja wa wakristo wote angalau sasa unaweza kufikiwa na kuendelea kung’aa. Watu wote wanaitwa wawe wapya na kitu kimoja, wakimkiri Yesu Bwana na mwokozi mmoja, wakikiri imani moja na kusherehekea fumbo la imani la Ekaristi.'



Danieli 7: 25
“Naye atanena maneno kinyume chake Aliyejuu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliyejuu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati na nyakati mbili na nusu wakati”


'Ni wazo kubwa: Mpango mpya wa dunia, ambapo mataifa yataunganishwa pamoja chini ya sababu moja…Ni Marekani pekee yenye mbinu na msimamo wa kimaadili kuuwezesha' - Hotuba ya George Bush -Los Angeles Times Feb. 18, 1991

'Marekani itakapoitawala dunia, Kanisa Katoliki litatawala duni' - Askofu Mkuu Quigley, 1903, The Chicago Tribune

'Wito wa Utawala Mpya wa Kimataifa watolewa kwa ajili ya Amani'

Yatokeapo haya Yesu asema:

“Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu” - Ufunuo 14:12


“…Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake” - Ufunuo 18:4

4 comments:

  1. THATS GREAT UDSM KEEP IT UP, MOTO HUO MLIOWASHA NAOMBA MUNGU KWA NEEMA YAKE ATUWEZESHE KUUSAMBAZA NCHI NZIMA NA DUNIA YOTE IMWONE YESU

    ReplyDelete
  2. may God bless you guys so that you may keep revealing the truth about the true God and Sabbath.

    ReplyDelete
  3. Ni vema kusema ukweli kwani wengi wanao jiita watumishi wa Munga wana ficha ukweli na kuambia watu habari za uponyaji na utowaji ili wawe na pesa ila mtumishi wa kweli ni lazima afundishe mambo yote hasa hili la mnyama katika siku za mwisho tunaitaji mafundisho kama haya ili tujuwe jinsi ya kuepuka

    ReplyDelete
  4. Haya ndio mafundisho tunayo itaji sana kwani huu ndio wakati wake sio wengine wanakaliya miujiza, kubarikiwa na utoaji ili wapate pesa asante sana MUNGU awe Nanyi Daima na hubuma hii iende mbele ili watu wajuwe ukweli

    ReplyDelete