Loading...

Tuesday, May 3, 2011

Waumini Wazidi Kuongezeka Kanisani Ikizu

Wanafunzi 111 walibatizwa kwenye juma la maombi lililoendeshwa na Mchungaji Gerald Nyakrere, Mchungjai Shukurani Mutaki na Mchungaji Daudi Ndekeja katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ikizu. Kutokana na ongezeko la wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Ikizu Kanisa dogo lililojengwa zamani sasa halitoshi. Hivyo wanafunzi wanasalia nje wakati wa ibada kama inavyoonekana pichani wakati wa huduma ya Ubatizo. Picha hizi zilizotumwa mtandaoni na Baraka Joel Nyakrere ni changamoto tosha kwa Wanafunzi wa zamani wa Ikizu na marafiki wote wa Kanisa la Ikizu kusaidia ujenzi wa kanisa kubwa zaidi litakalotosheleza mahitaji ya waumini wapya.

No comments:

Post a Comment