"Nimefurahi kusikia upo Mombasa. Ikiwezekana, fika pale Tononoka Grounds, kuna kanisa jipya tumeanzisha pale. Mwaka 2009 tulifanya efoti pale na kubatiza watu zaidi ya 500. Mwaka uliofuatia, tukanunua jengo kwa Shs. za Kenya milioni 12. Mwaka jana tukazindua kanisa katika Jengo hilo. Mwaka huu, tumenunua redio iliyokuwa inajulikana kama Shake FM 106.5 kwa gharama ya milioni 18 za Kenya, na hivi sasa redio hiyo imehamishiwa katika ghorofa ya kwanza ya jengo tulilonunua kwa ajili ya kanisa na matumizi ya redio na television. Nitafurahi ukipiga picha za redio na jengo hilo ili kuwatia hamasa watu wa Mungu tulio wasafiri. Waambie umetokea Dar Es Salaam, watafurahi kukupokea" - Msafiri Mwadventista, 18 OKTOBA 2011
"Mtu wa kwanza kabisa kunipa salamu zako ni kijana Samweli Machio. Hilo ni jina lake tangu utotoni. Huyu alikuwa kijana wa mtaani “chokoraa” kwa miaka zaidi ya 25. Hakuwahi kuishi ndani ya nyumba kwa maisha yake yote. Alimpokea Yesu kwenye effort yenu akabatizwa na kuacha aina zote za uvutaji, sasa ndiye mwangalizi wa kanisa kama alivyokuwa Samweli mwenyewe. Picha yake akiwa ndani ya kanisa amemaliza kuandaa kwa ajili ya ibada ya jumatano."
"Salamu za pili ni kutoka kwa wazee wawili wa kanisa. Elder John Maxwell na mwenzake. Waliotumwa na kanisa kuja DSM kukutafuta kwa ajili ya zoezi gumu la kupata mamilioni ya pesa ulizoelezea kwa ajili ya kununua hilo jengo. Walikuja DSM bila kujua wanakokwenda .... Wamenieleza jinsi Mungu alivyokuwa upande wenu hadi hilo jengo likanunuliwa na kanisa badala ya kununuliwa..."
"Salamu za tatu ni za Pr. Silas Saro. Amefurahi sana kusikia kwamba umeniambia nifike hapo. Wako kwenye ukarabati wa kituo cha redio kilichokumbwa na mvua na maji kujaa kwenye studio na kufanya uharibifu mkubwa. Pichani utaona studio iliyokuwa ikitumiwa imeharibika, maji yalijaa ndani na kukatisha matangazo kwa muda. Hivi sasa wamehamishia kila kitu kwenye chumba kingine na wanafanya ukarabati wa jengo juu ili mvua isiendelee kuleta maafa kwao. Matangazo yanaendelea kama kawaida..."
"Salamu za nne ni kutoka kwa Bw. Shabaan Ndege. Mkurugenzi mkuu wa kituo cha Sheki FM 106.6. Aliyekuwa mtangazaji wa UHURU radio inayomilikiwa na Mhe. Raila Odinga na kusikika nchi nzima. Huyu bwana baada ya kuombwa na kanisa akaacha kazi kwa Raila na kuanza kuitumikia radio ya kanisa. Kwa wanaoangalia TBC1 mtamkumbuka, alikuwa na Tido Mhando akitangaza kutokea Nairobi. ....Wamenionyesha mipango ya kukipanua hicho kituo, wanahitaji maombi mengi..."
No comments:
Post a Comment