GLOBAL YOUTH DAY (GYD): 18/03/2017
Siku ya vijana ulimwenguni kama inavyojulikana kwa Kiingereza kama Global Youth Day (GYD) ilisherehekewa mwezi uliopita na vijana wa kiadventista ulimwenguni kwa vijana wa umri tofauti tofauti kushiriki kufanya matendo mbali mbali kwa ajili ya kuigusa jamii inayowazunguka. Siku hii yenye lengo la kuwataka vijana waoneshe matendo yanayomhubiri Yesu yamepewa moto uitwao 'Uwe hubiri' yaani 'Be the Sermon' kwa lugha ya Kiingereza.
Siku hii yenye mguso wa kipekee kwa vijana ilizinduliwa na kanisa la wasabato ulimwenguni mnamo tarehe 13 Mwezi wa tatu mwaka 2013, na kuanzia hapo kila mwaka uliofuata vijana wamekuwa wakifanya shughuli mbali mbali katika wiki hiyo kuifikia jamii kwa matendo ya huruma.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio kwa picha yaliyofanywa na baadhi ya vijana wadogo ili kuwafikia watu mbali mbali na kuwa hubiri kwao kupitia matendo yao.
Ukipenda kutembelea matukio mbali mbali ya siku hiyo ya vijana ulimwenguni kupitia mitandao ya kijamii unaweza tembelea mitandao katika kiunganishi hiki au kwenye twitter kupitia hashtag #GYD17
No comments:
Post a Comment