Loading...

Tuesday, March 27, 2012

SAFARI YENYE MATUMAINI

"Safari Yenye Matumaini"

Elias Wankyo

Isaya 43:18 "Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno (jambo) jipya" "Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani."

New King James Version. Isaiah 43:18,19 "Do not remember the former things, nor consider the things of old. Behold, I will do a new thing" "I will even make a road in the wilderness and rivers in the desert."

Katika nchi ya Colombia kule Amerika ya Kusini mwanamke mmoja aitwaye Ingrid Betancourt aliamua kugombea Uraisi wa nchi hiyo. Katika mojawapo ya kampeni zake alitekwa nyara na kundi moja la ugaidi nchini humo. Kwa hali ngumu na ya kusikitisha alichukuliwa mateka na baadhi ya kundi lake na wakafichwa kwa muda wa miaka sita. Lakini mwaka 2008 mwishoni, Majeshi ya Serikali ya Colombia yalivamia maghaidi hao na kumkomboa Ingrid na watu wake wote wakiwa hai.

Ingrid aliporudi nyumbani salama alilakiwa na watu wakiwemo ndugu na jamaa zake. Ingrid akaenda mara moja kwa mama yake akamkumbatia kwa furaha iliyo kuu, na mbele ya waandishi wa habari akasema maneno haya mazito ambayo niliyaandika kuwa kumbukumbu nilipoyasikia kwenye taarifa ya habari:"Don't cry for me now. You don't have to cry for me anymore". Kwa Ingrid, inaonekana alikuwa tayari kufunga kitabu cha historia ya miaka 6 alipokuwa mateka, na kwa vile alikuwa huru sasa, alimwambia mama yake na watu wake, sasa kulia kwa ajili yake kungefikia mwisho, wafunge kitabu hicho kabisa, waanze maisha upya na waendelee na "Kitabu" kipya cha maisha.

1) Safari yenye matumaini inahitaji tusiwe watumwa (au kufungwa kama tuko jela) kwa uzoefu au mambo mabaya katika maisha yetu yaliyokwishapita. (Not to be prisoners of our negative "experiences" in the past).

Kila mwanadamu katika maisha amepitia hali fulani ngumu katika maisha, ila hali hizo zinatofautiana kati ya mtu na mtu. Kuna wengine ambao uzoefu au hali waliyopitia ni ngumu sana na imesababisha majeraha na makovu makubwa. Kwa sisi Waadventista tukikutana kanisani siku ya Sabato, hasa makanisa ya mijini, tumekuwa tumevaa vizuri, na kawaida tukiulizana, "habari gani?" Jibu la rahisi huwa kwa kawaida, "Ni nzuri". Lakini kwa ujumla tunaweza tusijue watu wanayopitia katikati ya wiki, au kwa ujumla katika maisha yao.

Nilikuwa katika mahubiri ya hadhara (Public Evangelism), Mhubiri alipotoa wito, nikashuka jukwaani, kuwapa mkono na kuwakaribisha walioitikia wito. Mama mmoja akasogea mbele akiwa na mnyororo mkubwa shingoni na mikononi. Nikamkaribia ili nijue alikuwa na nia gani. Kwa bahati mbaya hatukelewana kimazungumzo na hakuwa tayari kunisikiliza, ikabidi shemasi amchukue kwenda pembeni ya mkutano. Lakini suala hilo likawa kichwani mwangu kwa muda mrefu. Mfano mwingine, Sabato moja, niliomba watu walio na maombi maalumu waje ofisini kwangu baada ya ibada ili tuombe pamoja. Watu kadhaa walikuja. Mmoja wa waliokuja, alikuwa amempoteza mke wake kwa kifo mwaka uliokuwa umepita, na kipindi hicho, ndicho kilikuwa memorial anniversary.

Ilipofika zamu yake alisema, wiki hii nimekuwa nikitafakari kujiua kwa kumkumbuka mke wangu aliyefariki. Nilishikwa na mshangao mkubwa, ila nilificha moyoni mwangu kama kiongozi, ili nimpe matumaini na kuomba naye pamoja na kundi lililokuwa limekuja. Namshukuru Mungu kuwa Mzee huyo alipata matumaini kwa Bwana Mungu na aliendelea kuishi. Ninapotoa kisa hiki, ninakumbuka miaka yangu ya kuhudumu kule Texas miaka ya nyuma, lilikuwa ni kanisa dogo. Baadaye nikahamia State nyingine. Baada ya muda kadhaa, nikakutana na washiriki wawili kutoka kanisa lile dogo kule texas. wakanipa taarifa kuwa mama... mama fulani) alijiua. Nikaumia sana moyoni mwangu. Nikajiuliza, je nilipokuwa kule kuna jambo ambalo ningemsaidia huyo mama ambalo lingempa tumaini la kuishi. Je, katika mahubiri au mafundisho yangu ya Biblia, ni jambo gani ambalo ningelitoa ambalo lingemsaidia hata baada ya miaka kupita lingempa tumaini la maisha? Je, washiriki na viongozi wa kanisa hilo waliofuata, wangemsaidiaje huyo mama ili asifikie mahali na kukata tamaa ya kuishi?

Hali ya kukata tamaa sio ngeni. Tunakumbuka katika Agano la Kale kisa cha Musa alipotaka Mungu akatishe maisha yake, pia Nabii Eliya alipokuwa amekimbilia kwenye pango akiwa amekata tamaa ya maisha.

Kwa viongozi na washiriki wa Kanisa tuna majukumu makubwa, sio tu kwa ajili yetu wenyewe, bali pia na wale tunaokutana nao NDANI NA PIA NJE YA KANISA ili kujihimiza na pia kuwahimiza wengine ili kuendelea kuwa na matumaini kwa Mungu wa mbinguni katika safari ya maisha.

Mchungaji fulani katika conference fulani Amerika, alielezea kisa hiki kwenye mkutano wa Makambi: Alipokuwa Mchungaji kijana alitumwa kwenda kanisa fulani kuwa kiongozi hapo. Mara tu baada ya kufika mshiriki mmoja akaja kulalamika kuwa mwaka wa 1963 mshiriki mwingine alimtendea jambo baya sana. Huyu mchungaji kijana akasema, "Ndugu yangu suala hilo liliwatokea kabla ya mimi kuzaliwa. Sasa unategemeaje mimi nije kulisuluhisha, baada ya wewe kukaa nalo miaka hii yote na mko kanisa moja? Huyu mchungaji alitoa kisa hicho kufundisha umuhimu wa msamaha wa kikristo (forgiveness in Christianity).

Ni muhimu kusamehe na kuendelea na maisha mbele, La sivyo tukikaa na mabaya kwa muda mrefu, yanafanya madhara kwetu wenyewe kuliko wale tunaowakasirikia. Hata kama yule aliyetukosea asirudi kuomba msamaha, au asikubali kuongea ili kusuluhisha suala na misamaha itokee, jukumu letu ni kusamehe. Ila haya hayawezekani, isipokuwa kwa maombi na unyenyekevu tukimruhusu Roho Mtakatifu aendelee kufanya kazi mioyoni na akilini mwetu.
2)Safari yenye matumaini inahitaji tuwe na imani kwa Bwana Mungu wetu kwa ajili ya mapya.

Katika mafungu ya Isaya hapo juu, Bwana anaahidi kutufanyia kitu na/au mambo mema mapya.

Tunakumbuka yale Bwana aliyotutendea katika maisha yetu, lakini, tusiishie kwenye kumbukumbu tu (Memories only). Tumuombe Bwana ili kwa huruma na neema yake atusaidie tulio viumbe wake tumuone akitenda mapya makuu katika maisha yetu ya kila siku. Ni rahisi sana yule adui shetani kuleta vurugu na mawimbi, na giza, ili kujaribu kutuzuia tusione kazi ya Bwana ya kila siku katika maisha yetu.

Wakati fulani nilimsikiliza mhubiri aliyekuwa amealikwa kama Guest Speaker, ambaye alikuwa former, then retired, General Conference Executive Secretary. Pastor R. akasema kuwa alipokuwa katika uongozi no. 2 Executive position kule GC Headquarter, alichokuwa akisema au kufanya, in Official Capacity, kilikuwa kinapewa uzito mkubwa unaostahili. Ila mambo yalibadilika baada ya yeye kutoka hapo ambavyo ni kama kawaida kwa kila uongozi. Ila akasema kwa kusisitiza, hataki kukaa na kumbukumbu ya 'position' hiyo ya juu tu na kuacha kumfanyia Bwana kazi hali akiendelea kuishi. Pastor R. alieendelea, "The things we do for the Lord may not be written in the Adventist Review, other Church Journals, or even receive, "Thank You Notes" from others, but we must continue to do them, because we are doing for our Lord and Saviour Jesus Christ and His people". "Jesus has done a lot more for us. He gave His own life for our redemption".

3)Safari yenye matumaini inahitaji tumtumaini Bwana kwa ajili ya maisha yetu yajayo.

Yeremia 29:12. "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho."

Katika mafungu ya Isaya 43:18-20 Bwana hakuahidi kuondoa misitu wala kuondoa majangwa katika maisha. Ila Mungu wetu ameahidi kuwa ataweka njia au barabara njema wakati misitu ikiendelea kuwepo, na ataweka maji mazuri wakati majangwa yakiendelea kuwepo.

As we travel through this New Year 2012, we have left the past, we are presenting our present, and committing our future in God's continued loving care, mercy, guidance, protection and the in-working of the Holy Spirit. In Him we live and move and have our being. "We have nothing to fear for the future, except as we shall forget the way the Lord has led us and His teachings in our past history" (EGW, Life Sketches, page 196).

Elias Wankyo

14 January 2012

No comments:

Post a Comment