Loading...

Saturday, June 29, 2013

Mahubiri Star TV: "Kweli Itakuweka Huru"

Yale mahubiri yetu kwa njia ya Television ambayo yaliahirishwa wiki kadhaa zilizopita sasa yataanza rasmi siku ya Jumapili saa 9-10 STAR TV. Mahubiri hayo ni ya pekee sana na yametayarishwa kwa weledi wa hali ya juu ili kutofautisha na wale wenzetu.


Nimeambatanisa poster kama unaweza i-print na kuwasambazia watu. Tunatarajia wasabato wote watuunge mkono katika mradi huu mkubwa. Kama tulivyoaeleza hapo nyuma ni gharama sana kurusha vipindi hivi, lakini hatuna hofu kwani Mungu wetu ndiye mwenye fedha na dhahabu zote ulizonazo na alizonazo mwingine. Tumedhamiria kuendelea na vipindi hivi kwa wiki 28 ili mafundisho yote ya kanisa yapate kuwafikia watu kwa ukamilisfu.

Tunahitaji support yako kwa kualika marafiki zako kusikia habari hizi njema, na pia kusaidia fedha ili vipindi hivi visikwame. Kwenye hivyo vipindi tumeweka namba za simu kwa ajili ya kuchangia. Tuma m-pesa, tigo pesa ama airtel money, iwe ni 1,000, 2,000, 3,000, 10,000, 50,000, 500,000, 1,000,000 na kadhalika. Imani yetu ni kuwa pesa yako haitaenda bure, kwanza kuna mtu fulani ataokolewa na pili Mungu atakulipa.

[Namba zenywe ni hizi zifuatazo:


Tigo Pesa       0656 883317

M-Pesa           0757 402339
Airtel Money  0684 334416

Kuthibitisha kuwa unatuma mahali sahihi hakikisha kina la Ushindi SDA linaonekana]

Kwa wale walio nje ya nchi ama hata ndani ya nchi wanotumia mtandao tuna habari njema kwenu, mahubiri haya yatapatikana pia katika YouTube. Utafungua website ya kanisa www.ushindisdachurch.org hapo utapata link itakayokupa mahubiri haya kila wiki. Waambie na marafiki zako ili popote pale kiswahili kinaposikika ulimwenguni ujumbe ufike.


MUNGU AKUBARIKI SANA UNAPOJIANDAA KUUNGA MKONO JUHUDI HIZI ZA KANISA LA USHINDI.  NA NYOTE POKEENI BARAKA ZA BWANA.


MATHIAS MAVANZA

MZEE WA KANISA, USHINDI SDA CHURCH

No comments:

Post a Comment