Thursday, July 16, 2009

Mchungaji Kisaka (Mzee Tulia kwa Yesu) Amepumzika

Tumepokea kwa masikitiko taarifa za msiba wa Mchungaji wetu Mpendwa Dakta John Kisaka maarufu kama Mzee Tulia kwa Yesu. Ni imani yetu kuwa Mrisha Kisaka ametulia na Yesu katika Tumaini lenye Baraka. Kama Ufunuo 14: 13 inavyosema: "Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao." Amen.

Ifuatayo ni taarifa ya msiba kama ilivyowasilishwa kupita katika mtandao wa Tanzania Adventists in the United States (TA-US):

Ndugu na Dada katika Kristo,

Habari zimetoka Nairobi kuwa Pastor wetu Dr. John Kisaka amefariki kule Nairobi Hospital. Dr. Kisaka alikuwa Nairobi Hospital kwa matibabu. Kwa Wana-Taus tunamkumbuka Pastor Kisaka kwa mahubiri aliyokuja kufanya hapa na hadithi tamu na nzuri na maombi yake kwa ajili yetu. Baadhi yetu Dr, Kisaka alitufundisha kule USA RIVER, Arusha wakati shule yetu ya Waadventista ikiitwa TASC ambako kulikuwa na wanafunzi kutoka Tanzania, Kenya, na Sudan.

Baada ya kumaliza Doctoral Program katika Ministry kule Andrews University, Dr. Kisaka alirudi Tanzania ambako alifanya kazi katika Tanzania Union of the Seventh-day Adventist Church. Alifanya kazi kama Principal na lecturer Tanzania Adventist & Seminary, USA RIVER, ARUSHA. Baadaye alikuwa Ministerial Director kwa Tanzania Union. Watu wengi walipenda mahubiri yake katika Makambi na pia ile Semina yake ya TULIA KWA YESU ambayo ilikuwa very popular na ilibariki watu wengi. Dr. Kisaka alifanya mahubiri yake pia kule Kenya, England, USA na kwingineko. Alikuwa na moyo wa kutembelea watu nyumbani na kuomba nao. Alipokuja USA kwa mara ya mwisho alikuja mpaka nyumbani kwangu tukazungumza na nakumbuka maombi specific aliyoniombea.

Mtumishi wa Mungu, ambaye alitoa maisha yake yote kumtumikia Mungu na watu wake, amepumzika katika kifo. The Apostle John in the book of Revelation wrote words that are applicable even now--Revelation 14:13 "And I heard a voice from heaven (from God) saying unto me, write, Blessed are the dead which die in the Lord from henceforth: yea, saith the Spirit , that they may rest from their labors: and their works do follow them. (KJV)

Sincerely,
Elias Wankyo

4 comments:

  1. We shall really miss and remember Dr. Kisaka for his sermons and verses like...Wana Amani nyingiiiii.....waishikao sheria ya Bwanaaaaa.....wala haaawana la kuwakwaza; Haleluyaaaa aaa Haleluyaaaaa.... Haleluya tumsifuuuuuuu. For your informatiom Magomeni SDA Church have beeen eve since conducting TULIA KWA YESU prayers every day morning at 5.30 a.m. under the good leadership of Elder Lazarus Mollel. I joined about a year ago and I have never been the same again. I invite anyone who can join .....be rest assured you will never be the same again

    Be Blessed

    Dorrothy A. Sekimang'a

    ReplyDelete
  2. duh ckufahamu hili mapema ndio nimeona leo 4/3/09.imetokea lini?nini ilikua tabu?wao nimeumia kuckia hilo lkn tutambue kwamba na cc njia ni hiyo hiyo.mie ni abihudi amani abymike

    ReplyDelete
  3. from annie!
    wasabato msiumie kwa hili la mc. kisaka jihurumieni kwa mioyo yenu migumu, ombeni roho mtakatifu je mmesoma lesson tunda la roho, mmekuwa wagumu wa mioyo, je huyu Yesu anngeitunza sabato kwa moyo mgumu angeweza kufa msalabani jirekebisheni muuteni roho mtakatifu mbadilike.

    ikumbuke siku ya sabato uitakase na roho mtakatifu ndiye yeye. amen

    ReplyDelete
  4. ITS SAD NEWS FOR ME TODAY 24.02.2010 TO LEARN DR KISAKA,S DEATH. HE HAS DONE THE BEST LET HIM REST IN PEACE. LYDIA UOA 2008 NURSING CLASS

    ReplyDelete