Loading...

Tuesday, May 8, 2012

Mahojiano Kuhusu Historia ya KanisaWajoli wa BWANA,

Ninawasalimu. 

Sabato ya jana ya tarehe 6,05,2012; nilibarikiwa sana kuabudu katika kanisa ambalo ni la kwanza kwa injili ya waadventista wasabato Ulimwenguni.

Nilialikwa na mwenyeji wangu ijumaa usiku ambaye aliniuliza kama ningekuwa radhi kwenda kusali kanisa la jirani. Nami sikusita maana huwa natamani kubadilisha mazingira, kama wengi wenu mnavyofanya. Ila sikufahamu kama kanisa tutakalokwenda, lina historia kubwa namna hii.

Tukiwa njiani siku ya sabato, alianza kunieleza historia ya kanisa hili, ambalo limeachwa kama makumbusho kwa historia ya kanisa letu. Nilipata raha sana kusali kanisa alilowahi kusali mama Elen White, teh teh! nikahisi kama napata upako mpya. hahaah!

Nimejaribu kuchukua picha chache za maeneo ya hapo kanisani, na pia nilimuuliza mmishenari mmoja wa kanisa letu la keene, ambaye kwa kweli anaifahamu historia vizuri. Nikapata wazo la kurekodi sauti yake wakati tayari tukiwa tumeanza mazungumzo. Nimeattach hiyo video. haiko organized vzr, na haina viwango vyenu kabisa ninakiri hilo nanyi mtashuhudia, lakini natumai mtabarikiwa kwa ujumbe.

Nilipata fursa ya kuona makaburi ya waumini wetu waliolala mauti 1907, 186..., (pichani kwa majina zaidi). 

kumradhi tena, Picha zimefifia kdg, ni kutokana na kifaa nilichotumia. Natumai mtabarikiwa ktk unyonge wake.

Tujiunge ktk viambatanishi  vyangu dhaifu.

Mbarikiwe

JRuby.

No comments:

Post a Comment